Dodoma FM

Vijana waiomba serikali mikopo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi

16 October 2026, 16:36

Picha ni vijana wa wanaotarajia mikopo kutoka serikalini ili iwasaidie kufanya shuguli za maendeleo katika jamii. Picha na Habari leo.

Licha ya vijana kupewa elimu na kushiriki semina zinazolenga kuwahamasisha kutumia fursa za mikopo, bado baadhi yao hawajachukua hatua za kujiunga katika vikundi ili kunufaika na mikopo hiyo na kuanzisha miradi ya kujipatia kipato.

Na Victor Chigwada

Licha ya vijana wengi kuhitimu elimu ya juu, ukosefu wa ajira bado ni changamoto inayowakabili, hali iliyowafanya baadhi ya vijana Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kuitaka Serikali kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha kupata ajira na kutumia ujuzi walioupata kujikwamua kiuchumi.

Wakizungumza na Taswira ya Habari, vijana hao wamesema pamoja na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kujiajiri, bado kuna haja ya kuwepo kwa mikakati zaidi ya kupanua fursa za ajira kwa wahitimu wa vyuo mbalimbali.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo wa Kata ya Ng’hambaku, Richard Kisubi, amesema mikopo hiyo inalenga kuwawezesha vijana kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi, lakini mwitikio umekuwa mdogo kutokana na baadhi yao kushindwa kuunda vikundi vinavyohitajika ili kunufaika na fursa hizo.

Simulizi na Victory Chigwada.