Dodoma FM
Dodoma FM
12 May 2026, 16:36

Aidha ametoa wito Kwa Wananchi kuzingatia taratibu za kisheria Ili kupunguza migogoro au kuepuka kuingia Katika makosa ya jinai.
Na Stephen Noel .
Wananchi wa wilaya ya Mpwapwa wamejitokeza kupata msaada wa kisheria unaotolewa na timu ya mama Samia Legal Aid Katika viwanja mashujaa .
Wakiongea na Taswira ya habari wananchi hao wamesema watu wengi wanakabiliwa na changamoto ya migogoro ya ndoa ,Ardhi na mirathi hivyo kusogezewa huduma ya msaada wa kisheria karibu itawasaidia kutatua kero hizo.
Aidha baadhi ya wanawake wamesema migogoro mingi ya ndoa katika eneo hilo inatokana na wanawake kujiingiza katika mikopo umiza maarufu kama kausha damu bila kuwashirikisha wenza wao na kujikuta wakipoteza vitu.
Jene mbelwa mmoja wa wanasheria katika walipo katika eneo hilo la Mpwapwa amesema uelewa mdogo wa Sheria Kwa Wananchi hupelekea baadhi kupoteza Haki zao za Msingi .