Dodoma FM
30 June 2026, 17:27

Mwana fahari bado tupo kijiji cha farkwa wilayani chemba ambapo wakazi wa eneo hili ni watu wa asili ya kabila la wasandawe.
Na Yussuph Hassan.
Katika simulizi ya aina mbalimbali ya ngoma za kabila hili la wasandawe wanasema kwa sasa wanaweza kucheza ngoma hii ya Simboo kama burudani japo hapo zamani ngoma hii ilichezwa na watu wenye mashetani pekee.
Wazee wa kabila hili wanasema kwao ngoma huchezwa wakati wote wa furaha na rika mbalimbali hushiriki katika upigaji na uchezaji wa ngoma hizo isipo kuwa wakati wa majonzi.