Dodoma FM
Dodoma FM
16 April 2026, 4:12 pm

Ripoti hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi katika vijiji ishirini vilivyo ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Na Kitana Hamis.
Wilaya ya Kiteto imetangaza ripoti maalum ya mpango wa matumizi bora ya ardhi, ikiwa na lengo la kupunguza migogoro ya ardhi katika vijiji ishirini. Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Obeid Kamonge, amesema mpango huo umefanikiwa kutoa elimu na kuainisha maeneo ya wakulima na wafugaji.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Remidius Mwema, amesema ripoti hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi katika vijiji ishirini vilivyo ndani ya halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Aidha, Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa wilaya tano mkoani Manyara zinazokabiliwa na changamoto za migogoro ya ardhi. Hivyo, mpango huu wa matumizi bora ya ardhi unatarajiwa kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza migogoro.