

19 June 2025, 4:55 pm
Jumla ya wafanyabiashara 30 wa kariakoo ambao ni washindi wa Tuzo za kariakoo wamewasili leo Jijini Dodoma baada ya kupokea mwaliko wa kushiriki vikao vya bunge na watatembelea Miradi mbalimbali katika Jiji la Dodoma.
Na Seleman Kodima.
Wafayabiashara wa Soko la Kariakoo wametajwa kuwa na Mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Nchini Tanzania soko kubwa na linalofanya vizuri ni Kariakoo lakini kwa sehemu kubwa wafanyabiashara hawa wanasahaulika kwenye eneo la kupongezwa na kwa jitihada wanazozifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo June 19 baada ya kuwasili Dodoma Mwazilishi Wa Tuzo za Wafanyanbiashara Kariakoo Zakayo Shushu anasema lengo la Tuzo hizi ni kusaidia wafanyabiashara kutambulika kwa jamii na kutambua mchango wao katika uchumi wao.
Baadhi ya wafanyabiashara wanasema hii imekuwa ni fursa ya kipee ya kuwapa hamasa pamoja na kuamika kwa jamii huku wakiomba marekebisho ya wafanyabiashara wageni kuingilia biashara za wafanyabiashara wa Ndani.
Cornel Kyai Ni afisa mwandamizi Shirika la Reli Tanzania amewakarishisha wafanyabiashara kufanya biashara zao katika Jengo la Stesheni.