Wazazi watakiwa kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya mitandao
14 May 2026, 16:38

Vile vile kupitia sheria ya mtoto kifungu cha 9 kinaeleza wajibu wa mzazi au mlezi kumlinda mtoto dhidi ya ukatili,udhalilishaji na mazingira yanayoweza kumdhuru.
Na Jerome John.
Wazazi na walezi mkoani Dodoma wamekumbushwa kuendelea kuwalinda watoto wao dhidi ya matumizi yasiofaa ya mitandao ya kijamii.
Kwa mujibu wa sheria ya mtoto wazazi,walezi na jamii kwa ujumla wana wajibu wa kumlinda mtoto kwenye mazingira ya kidigitali yasiweze kumuathiri.
Kupitia sheria hiyo Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi na afisa dawati la jinsia na Watoto Dodoma Michael Mkinda ameitaka jamii kwa ujumla kuzingatia matumizi ya mitandao ya kijamii wanayo itumia bila kuwaathiri watoto.
Aidha amesisitiza kuwa kusambaza picha au video ya mtoto akiwa uchi, mazingira ya fedheha, kuchapisha taarifa binafsi za mtoto zinazoweza kuhatarisha maisha yake Pamoja na kumrekodi akiadhibiwa ni kosa kwa mujibu wa sheria kifungu cha 158(1)(a) na (c).