Mkenda ataka sayansi ilete matokeo kwa wananchi
3 July 2026, 11:53

Taasisi hiyo itaendelea kuunganisha utafiti, ubunifu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku Mfumo wa NISSTI ukitarajiwa kuwa jukwaa la kuwaunganisha watafiti na wavumbuzi nchini.
Na Mariam Kasawa.
Serikali imesema ni wakati wa kutathmini matumizi ya rasilimali zinazowekezwa katika utafiti na kuhakikisha matokeo yake yanachangia kuvutia uwekezaji na kutatua changamoto za maendeleo nchini.
Hayo ameyabainisha na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, wakati akizindua Maadhimisho ya Kitaifa ya Miaka 40 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Mfumo wa Taifa wa Taarifa za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (NISSTI).
Prof. Mkenda amewataka watafiti, wavumbuzi, taasisi za utafiti na wadau wote kujisajili katika mfumo huo ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na fursa za ushirikiano.
Aidha Prof. Mkenda amesisitiza umuhimu wa vijana kuikumbatia sayansi na teknolojia kama njia ya kujenga ajira na uchumi shindani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu, amesema taasisi hiyo itaendelea kuunganisha utafiti, ubunifu na maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku Mfumo wa NISSTI ukitarajiwa kuwa jukwaa la kuwaunganisha watafiti na wavumbuzi nchini.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amesema maadhimisho hayo ni sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuifanya sayansi na ubunifu kuwa ajenda ya maendeleo ya taifa.