Dodoma FM

Wafungwa, mahabusu watakiwa kuutumia mwezi mtukufu kufanya toba ya kweli

8 April 2024, 5:48 pm

Pichani ni Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban akizungumza baada ya kukabidhi vyakula na vitabu kwa ajili ya futari kwa wafungwa na mahabusu katika gereza la Isanga jijini Dodoma.Picha na Seleman Kodima.

Shughuli hiyo iliratibiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA wilaya ya Dodoma kwa kushirikiana na misikiti ya wilaya ya Dodoma.

Na Seleman Kodima.
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban amewataka wafungwa na mahabusu waliopo magerezani kutumia vyema mwezi huu mtukufu wa Ramadhan kwa ajili ya kutubu na kuomba toba ya kweli ili Mwenyezi Mungu awasamehe katika adhabu zinazowakabili.

Hayo ameyasema jana wakati alipokabidhi vyakula na vitabu kwa ajili ya futari kwa wafungwa na mahabusu katika gereza la Isanga jijini Dodoma ambapo shughuli hiyo iliratibiwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA wilaya ya Dodoma kwa kushirikiana na misikiti ya wilaya ya Dodoma.

Akizungumza wakati akikabidhi Futari hizo,Alhaji Mustafa Rajab amesema ni muhimu wafungwa na mahabusu waliofunga kufuturu na kupata chakula kama ambavyo waliopo uraiani wanakipata.

Sauti ya Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shaban .
Picha ni Kamishina Msaidizi wa jeshi la Magereza na Mkuu wa Gereza kuu Isanga Dodoma Zephania Neligwa akiongea baada ya kupoea vitu hivyo kutoka kwa Shehe mkuu.Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wake Kamishina Msaidizi wa jeshi la Magereza na Mkuu wa Gereza kuu Isanga Dodoma Zephania Neligwa amesema mahitaji hayo yataenda kuwasaidia wanafunzi wao ambao ni wafungwa na mahabusi waliopo mafunzoni na wale ambao wamefunga mwezi mtukufu wa ramadhani.

Sauti ya Kamishina Msaidizi wa jeshi la Magereza na Mkuu wa Gereza kuu Isanga Dodoma