Dodoma FM

Maji yapelekea baadhi ya wakazi wa kata ya Nkuhungu kuyakimbia makazi yao

9 August 2021, 1:46 pm

Na; Fedrick Lukasho.

Wananchi wa kata ya Nkuhungu katika mitaa ya Mnyakongo ,Bochela, Mtube na Salama Jijini Dodoma wameiomba Serikali kutatua changamoto ya maji kutuama kwa muda mrefu katika makazi yao.

Wakizungumza na Dodoma FM Radio kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi hao akiwemo Mary John pamoja na God Sadlye wamesema changamoto hiyo imekuwa ya muda mrefu na imesababisha baadhi ya watu kuyahama makazi yao.
wamesema kutokana na adha hiyo imelazimu baadhi ya wanachi kuishi katika majengo ya shule ya msingi mnyakongo ambayo imeanza kujengwa hivi karibuni ili kuepuka madhara makubwa ambayo yanaweza kujitokeza.

Clip 1 Wananchi…………………

Dodoma FM imezungumza na mwenyekiti wa mtaa wa mnyakongo Bw. Hector Stephano na kueleza kuwa hadi sasa changamoto hiyo imefikishwa ngazi ya juu kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi.

clip 2 Mwenyekiti…………….

Amesema pamoja na hatua walizochukua lakini bado hakuna utekelezaji wowote ulioanza hivyo kupelekea wananchi wa eneo hilo kuwa na hofu ya mvua zinazo tarajia kuanza hivi karibu katika msimu wa masika.