Dodoma FM

Wajawazito watakiwa kufanya maandalizi mapema

21 September 2023, 4:38 pm

Wataalamu wa Afya wanashauri kuwa mama mjamzito anatakiwa kuwa na maandalizi kabla ya kujifungua.Picha na mama Afya Bora.

Wataalamu wa Afya wanashauri kuwa mama mjamzito anatakiwa kuwa na maandalizi kabla ya kujifungua kwani kuna umuhimu wa kufanya hivyo ili kuepukana na madhara mbalimbali yanayoweza kutokea.

Na Naima Chokela.         

Ushauri Umetolewa kwa Wajawazito  kuhakikisha wanafanya maandalizi kabla ya kujifungua kwani husaidia kulinda Afya ya mama pamoja na mtoto .

Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa afya ya mama na mtoto kutoka hospitali ya Makole Jijini Dodoma ,Ezeleda Elia wakati akizungumza na Dodoma fm ambapo amesema kuwa mama mjamzito anatakiwa kufanya maandalizi kabla ya kujifungua ili kuilinda afya ya mama pamoja na mtoto.

Sauti ya Ezeleda Elia .

Nao baadhi ya wananchi jijini Dodoma wamesema kuwa bado baadhi ya wanajamii hawana elimu juu ya umuhimu wa kuhudhuria kliniki ili kupata ufanisi wa maandalizi kwa mama mjamzito kabla ya kujifungua. 

Sauti za baadhi ya wananchi.