Dodoma FM

Muhimbili mbioni kuanza kutoa huduma za upandikizaji mimba

16 August 2023, 2:52 pm

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof Mohamed Janabi akiwa anazungumza na wanahabari Jijini Dodoma.Picha na Na WAF, Dodoma.

Amesema kuwa wataanza  na kliniki za kawaida kisha hatua za upandikizaji zitafutwa kwa kushirikiana na wataalamu elekezi kutoka nje ya nchi ili kufanyikisha huduma za upandikizaji mimba ambao wataelendelea kuwajengea uwezo wataalam wa Hospitalini.

Na WAF, Dodoma.

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iko mbioni kuanza kutoa huduma za upandikizaji mimba kwa mashine maalum (IVF – In vitro Fertilization)

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof Mohamed Janabi akiwa anazungumza na wanahabari Jijini Dodoma akielezea utekelezaji wa shughuli za Hospitali ya Taifa Muhimbili na mwelekeo wa mwaka 2023/24.

Prof Janabi amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekamilisha ununuzi wa mashine za kusaidia upandikizaji mimba zilizogharimu Shilingi Bilioni 1.

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan imekamilisha ununuzi wa mashine za kusaidia upandikizaji mimba zilizogharimu Shilingi Bilioni 1.

“Huduma  za upandikizaji mimba zitaanza kutolewa hivi karibuni baada ya  kamilisha usimikaji wa mitambo ya kutolea hizo” amesema Prof. Janabi

Picha ni waandishi wa habari na wadau wengine wakifatilia mkutano huo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dodoma. Picha na WAF, Dodoma.

Prof. Janabi ameeleza kuwa tatizo la watu kutopata ujauzito ni kubwa na Watanzania wengi wamekuwa wakitoka nje ya nchi kupata huduma za kupandikizwa mimba kwa gharama kubwa hivyo Serikali imesogeza huduma hizo karibu hivyo zitaanza kupatikana hapa hapa nchini.

Picha ni waandishi wa habari na wadau wengine wakifatilia mkutano huo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dodoma. Picha na WAF, Dodoma.

“Jengo limeshakamilika na Muhimbili tulitenga chumba cha kutolea huduma hizo na kwasasa tunasubiri usimikaji wa mitambo hiyo ikamilike ndo tuanze kutoa huduma hizo, na wananchi wanaohitaji huduma hizo hawata kwenda nje ya nchi kupata huduma hizo”, ameeleza Prof. Janabi.

Prof. Janabi amesema kuwa Hospitali tayari ina wataalamu waliowezeshwa na mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo na wamesharejea kutoka masomoni hivyo kusubiri kuanza kwa kutolewa kwa huduma hizo.