Dodoma FM

Wanawake watakiwa kuacha kukimbilia mikopo Mitaani

24 February 2023, 3:47 pm

Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri  ya Jiji la Dodoma Bi. Charity Sichona. Picha na George John.

Mikopo mingi ya mitaani imekuwa inapelekea kukosa faida na kushindwa kujiwekea akiba

Na Mariam Kasawa.

Wanawake wametakiwa kuacha kukimbilia mikopo ya Mitaani badala yake wajikite kuomba mikopo inayo tolewa na halmashauri ili waweze kunufaika na mikopo hiyo.

Akizungumza na Dodoma Tv Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri  ya Jiji la Dodoma Bi. Charity Sichona amesema  marejesho ya mikopo mingi ya mitaani imekuwa inapelekea kukosa faida na kushindwa kujiwekea akiba kutokana na marejesho.

Sauti ya Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri  ya Jiji la Dodoma.