Dodoma FM

Serikali yawataka maafisa biashara kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi

20 August 2021, 12:15 pm

Na;Mindi Joseph.

Serikali imewataka Maafisa biashara kufanya kazi kwa ushirikiano na weledi ili kuboresha huduma kwa wananchi na kupunguza kero pamoja na kuepuka kupokea rushwa.

Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo ya maafisa biashara Jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dotto James amesema mafunzo hayo yatawawezesha maafisa biashara kuwa mabalozi wa kuboresha mpango wa biashara Nchini.

Ameongeza kuwa mafunzo hayo yatakuwa chachu ya kupunguza kero mbalimbali za wafanyabiashara .

Kwa upande wake Kelvin Kalengela Afisa biashara Mlimba Dc amesema moja ya changamoto inayowakabili ni maafisa biashara kugeuka kuwa wakusanya mapato kwenye halimashauri zao.

Naye Mkurugenzi wa Leseni Bw. Andrew Mkapa ameahidi kwenda kufanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa kwao ili kutoa huduma bora kwa wananchi na wafanyabiashara.

Mafunzo ya maafisa biashara yameanza agosti 16 na yamefika tamati leo ambapo yamehusisha maafasi biashara kutoka Mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singinda.