Dodoma FM

Masumbwi wanawake kuahirisha mpambano.

19 March 2021, 1:04 pm

Na, Mariam Kasawa.

Pambano la  masumbwi kwa Wanawake Queen of the Ring (‘Malkia wa Ulingoni) limeahirishwa kupisha kipindi cha Maombolezo.

Mratibu wa Habari wa wakala wa Michezo Nchini wa  Peaktime Joyce Mbogo amesema  wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha  aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli kilichotokea tarehe 17machi  2021.

Alisema Msiba ni Mzito na Rais Magufuli atakumbukwa na wadau wa ngumi  kutokana na  Mapinduzi makubwa aliyoyafanya ya kutengeneza Kamisheni Moja kusimamia Mchezo huo.

Aidha alimpongeza Rais Mpya Mama Samia Suluhu Hassan na kumtakia kila la kheri katika majukumu mapya na kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Pia aliwataka mabondia watakaoshiriki pambano hilo watumie  kipindi hiki cha maombolezo kufanya mazoezi kujiandaa.

Aliwataja mabondia watakao wania mkanda wa dunia siku hiyo kuwa ni halima vunja bei atakayepigana na zulfa macho katika mchezo wa roundi 10.

Mabondia wengine ni Fatuma Yazidu  atakayepigana na Dorothea Muhoza, Happy Daudi dhidi ya Leila Yazidu na Lulu Kayage dhidi ya Jesca Mfinanga.

wengine ni Mwamne Haji  dhidi ya Sarafina Julius,Agnes Kayange dhidi ya Mwajuma Pengo,Grace Mwkamele dhidi ya Asha Gota wakati  Salma Kihombwa dhidi ya Mariam Mungi na Zawadi Kutaka  dhidi ya Martha Kimaro.