Dodoma FM

Leo tunaangazia uongozi kwa wanawake

13 December 2023, 8:39 pm

Picha ni Diwani wa kata ya Nala akiongea na Dodoma Tv. Picha na Fred Cheti.

Ameanza jitihada za kuhakikisha elimu inatolewa kwa wanawake.

Na Mariam Matundu.
Mifumo dume pamoja na uwoga vimetajwa kuwa sababu ya baadhi ya wanawake kushindwa kuwania nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali wakati wa chaguzi .

Diwani wa kata ya Nala bw. Hermani Masila amesema kuwa ameanza jitihada za kuhakikisha elimu inatolewa kwa wanawake ili waweze kuwania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024.