Watu wa karibu wanapambana vipi na vitendo vya ukeketaji
9 July 2026, 17:41

Tafiti nyingi zilizofanywa katika miaka ya hivi karibuni zinaonyesha hatua kubwa imepigwa kuwafungua wananchi juu ya mili hizo potufu,ingawa safari bado ni ndefu.
Na Mariam Matundu.
Serikali ya Tanzania imeanzisha mkakati wa kitaifa wa kutokomeza vitendo vya kikatili vya ukeketaji watoto wa kike, mkakati ambao pia unawajumuisha wahusika wa vitendo hivyo kama vile viongozi wa kimila.
Wanaofanya vitendo hivyo wanamini wako katika mkondo unaotambulisha mila na utamaduni , lakini kwa kutizama ukweli wa mambo, vitendo hivyo vinapora na kuutezwa utoto wa kike.
Mtoto wa kike aliyekeketwa kama anavyo wahi kusema aliyekuwa sema Naibu Waziri wa Afya, Mwanaidi Ali Khamis anapoteza thamani mbele ya uso wa jamii na kwa maana hiyo ile ndoto yake ya kufika mbali inapita kwenye mawimbi na misuko suko.
Wengi wanasema kwamba jamii iliyostarabika haiwezi kamwe kutupa wala kusau utamaduni wake, lakini utamaduni unaoonekana kufifisha maisha ya kundi fulani la watu ni umaduni uliopotea njia.
Kampeni hii ya kitaifa ina shabaha ya kuwafungua macho wale wanaoendelea kukumbatia vitendo hivyo kugutuka ili hatimaye washiriki juhudi za pamoja kumsaidia mtoto wa kike kukua katika malezi mema huku akiendelea kufurahia masomo.
Kwa vile elimu ni ufunguo wa maisha, bila shaka mangariba wanatajwa kuwa nyuma ya ukeketaji huo wanaweza kufuata uamuzi uliochukuliwa na ngariba mwenzao kama huyu ambaye sasa hayuko tena huko.