Dodoma FM

Pombe yapelekea wanaume kupata vipigo toka kwa wake zao

5 October 2022, 1:50 pm

Na; Benard Filbert.

Unywaji wa Pombe kupitia kiasi umetajwa kuchangia wanaume katika kijiji cha Kwa mtoro wilayani Chemba kupigwa na wanawake zao.

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanywa na Taswira ya Habari baada kufika kijiji hapo umebaini kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa wakifukuzwa na wake zao kutokana na unywaji pombe kupita kiasi.

Mwenyekiti wa kijiji cha kwa mtoro Bw Hussein Bakari chande   amekiri kuwepo kwa baadhi ya matukio hayo ambayo yanachangiwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuendekeza unywaji pombe pamoja na uvivu wa kufanya kazi hatua ambayo inawalazimu wanawake kubeba jukumu la kutunza familia .Clip mwenyekiti…………………..

.

Hata hivyo baadhi ya wanaume katika kijiji hicho wakizungumza na Taswira ya Habari wamekiri kuwepo kwa matukio hayo ingawa ni kwa uchache na mara nyingi vitendo hivyo vimekuwa vikijitokeza nyakati ambazo wakuu wa kaya wanapokuwa wamelewa.

.

Wakati matukio hayo yakitajwa kutokea katika kijiji cha kwa mtoro, Bi. Zainab Sungi ambae ni mkazi wa kijiji hicho amejikuta akibeba jukumu la kumle mjukuu wake ambae wazazi wake walitengana kutokana na ugomvi wa kifamilia.

.

Mwezi septemba mwaka huu Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kupitia mwenyekiti wa kamati hiyo stanslaus nyongo ilieleza  kushtushwa na kasi ya kuvunjika kwa ndoa nchini huku chanzo kikubwa kikiwa ni kumomonyoka kwa maadili na Mkoa wa Dar es Salaam pekee ukitajwa kuwa ndoa zaidi ya 300 zimekuwa zikivunjika kwa mwezi.