Dodoma FM

TPBRC yaandaa mapambano ya kuaza mwaka 2021

14 December 2020, 9:52 am

Bondia Ahmed Handy kushoto na Hamis Maya

Dar Es Salaam.

Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania TPBRC imeandaa mapambano kabambe ya ngumi ya kuanza mwaka.

Mapambano hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Valentine Februari 14,2021 katika ukumbi wa Viwanja vya Sabasaba jijini Dar Es Salaam.

Super D Kushoto akimkabidhi mkataba Bondia Ramadhan Mbegu “Migwedebaada ya kusaini

Mratibu wa mapambano hayo Rajab Mhamila “Super D” kutoka Super D Boxing Promotion amesema kutakuwepo mapambano manne ambapo:

Hamis Maya atapambana na Ahmed Handy pambano la raundi nane Kg.66.

Lingine ni kati ya Vicent Mbilinyi dhidi ya Ahmed Abdulrahim.

Naye Ramadhan Mbegu “Migwede” dhidi ya Hashim Kilanga kg.63 raundi nane huku Daudi Mwata akipambana na Abdul Ubaya pambano la raundi 6 kg.72.

Mwalimu wa Ndondi Rajab Mhamila