Dodoma FM

Wadau wa elimu wazungumzia mgawanyiko wa adhabu shuleni

23 December 2023, 4:35 pm

Picha ni baadhi ya wadau wakiwa katika ufunguzi wa Mradi huo. Picha na Seleman Kodima.

Ni ufunguzi wa mradi wa kuondoa ukatili dhidi ya watoto walioko shuleni ambao unaratibiwa na  mtandao wa Elimu TEMNET .

Na seleman Kodima.

Wadau wa Elimu wamesema kuwa ipo haja ya uwepo wa mgawanyiko wa adhabu kulingana na makosa yanayotendwa na wanafunzi ili kuweza kupunguza matumizi ya adhabu ya Viboko shuleni.

Hayo yamesemwa na wadau waliohudhuria ufunguzi wa mradi wa kuondoa ukatili dhidi ya watoto walioko shuleni ambao unaratibiwa na  mtandao wa Elimu TEMNET .

Akizungumza kuhusu adhabu ipi inafaa kwa Mwanafunzi Mbunge wa Viti Maalum Neema Gerrad amesema  wadau wanatakiwa kufahamu ni makosa yapi yanapatikana maeneo ya shule na kuanisha adhabu zake

Sauti ya Mbunge wa Viti Maalum Neema Gerrad

Picha ni Mbunge wa Viti Maalum Neema Gerrad akiongea wakari wa ufunguzi wa Mradi huo. Picha na Seleman Kodima.

Kwa upande wao TEMNET kupitia Afisa Mradi , Keneth Nchimbi     amesema kuwa Msimamo wa mtandao huo katika adhabu ipi bora kwa mwanafunzi  inajikita zaidi katika miongozo iliyotolewa na serikali kuhusu aina ya adhabu zinazotolewa .

Sauti ya Afisa Mradi , Keneth Nchimbi

Nao baadhi ya washiriki wa mradi huo,wamesema matumizi ya Viboko kama sehemu ya adhabu inatokana na sababu mbalimbali zinazosababisha na Malezi ya wazazi kwa watoto wao .

Sauti za wadau