Dodoma FM

Halmashauri ya jiji la Dodoma kupunguza adha ya madawati shuleni

23 March 2023, 12:29 pm

Baadhi ya mafundi wakiendelea kutengeneza madawati hayo.Picha na Fred Cheti.

Mkakati huo utasaidia kupunguza adha ya madawati inayo zikabili shule nyingi jijini Dodoma

Na Fred Cheti.

Halmashauri ya jiji la Dodoma imepanga kutengeneza madawati na kuyagawa kwa shule zote za serikali za Msingi na Sekondari zilizopo jijini hapa ili kupunguza adha ya wanafunzi kukaa chini.

Mkatakati huo unatekelezwa na halamshauri ya jiji la Dodoma kwa kushirikiana na jeshi la magereza ambao ndio watengenezaji wa madawati hayo kama anavyobainisha Afisa elimu Msingi na awali katika jiji la Dodoma Bi Prisca Myalla.

Sauti ya Afisa elimu Msingi na awali katika jiji la Dodoma Bi Prisca Myalla.
Madarasa ya shule ya Msingi Amani iliyopo Mlezi jijini Dodoma. Picha na Fred Cheti.

Kazi hiyo ya kutengemeza Madawati inafanywa na jeshi la Magereza katika kiwanda cha jeshi hilo kilichopo Msalato ambapo hapa Inspekta Jofrey Mganga kutoka jeshi la Magereza anaeleza mwenendo wa utekelezaji wa jambo hilo.

Sauti ya Inspekta Jofrey Mganga .

Miongoni mwa Shule zilizonufaika kwa kupatiwa madawati hayo ni Shule ya Msingi Mlezi kama anavyozungumza Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl. Anicetus Lymo.

Sauti ya Mwalimu mkuu wa shule hiyo Mwl. Anicetus Lymo.