Dodoma FM

Nini kinapelekea baadhi ya wazazi kutelekeza familia

13 September 2023, 4:59 pm

Picha ni diwani wa kata ya Bahi akiwa pamoja na viongozi wengine katika mjadala wa wazi ulio fanyika eneo la Bahi sokoni wilayani humo.Picha na George John.

Leo mchanyato upo Bahi kuzungumza na Jane Mgidange ambaye  ni mratibu wa Elimu jumuishi Wilaya Ya Bahi Kufahamu zaidi nini sababu za  kutelekeza familia.

Na Leonard Mwacha.

leo tunaangazia sababu za kutelekeza familia ambapo jamii inahusika moja kwa moja kabla ya kupata kufahamu zaidi tungefahamu kwanza nini maana yaKutelekeza watoto  ambapo imefafanuliwa kama “aina ya unyanyasaji ambao unamaanisha kutompa mtoto huduma ya malezi inayohitajika na inayostahili kulingana na umri wa mtoto ingawaje kifedha mlezi au mzazi anaweza kufanya hivyo.”

Mara nyingi watu hushindwa kutofautisha kati ya umasikini na kutelekeza watoto, kwa kawaida Familia masikini hazina uwezo wa kutoa huduma ya kutosha kwa watoto wao ila wazazi na walezi waliotelekeza watoto huwa na uwezo .