Dodoma FM

Km 19 za barabara kujengwa katika mitaa zaidi ya minne Makulu

12 October 2023, 12:40 pm

Picha ni Barabara hiyo mpya iliyojengwa katika kata ya Makulu Jijini Dodoma. Picha na George John.

Tayari wananchi waliopisha ujenzi wa Barabara hizo wameshalipwa stahiki zao.

Na Mindi Joseph.

Kilomita 19 za barabara zinatarajiwa kuchongwa katika zaidi ya Mitaa 4 katika Kata ya Dodoma Makulu kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Hii ni kufuatia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayounganisha kata 3 ikiwemo  kata ya Dodoma Makulu uliogharimu zaidi ya shilingi bilion 10 kukamilika.

Picha ni Diwani wa kata ya Makulu. Picha na George John.

Taswira ya Habari imezungumza na diwani wa kata ya Dodoma Makulu Mh. Fadhili Chibago hapa anaeleza kuhusu ujenzi wa barabara hiyo.

Sauti ya Mh Fadhili Chibago.

Maboresho katika barabara hiyo yanaendelea ikiwemo kuweka alama za watembea kwa miguu ili kuepusha Ajali.

Sauti ya Mh Fadhili Chibago.