

4 June 2025, 5:34 pm
Ikumbukwe kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan mikopo ya halmashauri ya asilimia 10 imeendelea kuwa mkombozi kwa wananchi.
Na Lilian Leopold.
Wananchi wa kata ya Kizota halmashauri ya Jiji la Dodoma wameeleza kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri kwa makundi ya wanawake , vijana na watu wenye ulemavu.
Wakizungumza na Taswira ya habari baadhi ya wanufaika hao wamesema mikopo hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao kwani umewasaidia kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii kata ya kizota Bi Theresia Ntui amesema kata hiyo imepokea jumla ya shilingi 410 ambapo vikundi vya wanawake vimepokea shilingi milioni 192 , vikundi vya vijana vimepata shilingi milioni 164 na watu wenye ulemavu wamepata milioni 49.