Changamoto ya umeme yakwamisha maendeleo kata ya Loje Chamwino
2 February 2023, 2:01 pm
Kuanguka kwa nguzo za umeme katika baadhi ya maeneo yenye huduma ya umeme katika kata ya Loje imetajwa kusababisha kukosekana kwa kuhuduma hiyo .
Na Victor Chigwada
Wananchi wa kijiji cha Ingunguli Kata ya Loje Wilaya ya Chamwino wameiomba Serikali kuwasambazia huduma ya umeme katika vitongoji vyao ili kuondokana na adha ya matumizi ya huduma hiyo
Hamisi Msangi ni mwenyekiti wa kijiji Ingunguli amesema kuwa pamoja na baadhi ya vitongoji kukosa huduma hiyo lakini changamoto nyingine ni kuanguka kwa nguzo za umeme maeneo yenye huduma hiyo.
Naye Diwani wa Kata ya Loje Bw.John Njohoka amekiri upatikanaji wa huduma ya umeme kwa kijiji cha Igunguli bado ni hafifu licha jitihada zinazo endelea kufanywa ikiwemo kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wananchi