Dodoma FM

Udugu na Umoja wadhihirika Zanzibar leo

23 March 2021, 10:24 am

Na; Mariam Kasawa

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania hayati  Dkt.John Magufuli utalala Ikulu Zanzibar leo Jumanne Machi 23, 2021 na kesho asubuhi utapelekwa Mkoani Mwanza.

Hayo yameelezwa leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokuwa kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar inakofanyika shughuli ya kumuaga Hayati Dkt.John Pombe Magufuli.

Amesema Zanzibar wananchi watapata fursa ya kila mmoja kupita kumuaga zoezi litakalo hakikisha kila mwananchi alie fika eneo hilo kuaga baada ya hapo Mwili utalala katika ikulu ya Zanzibar.

Akielezea ratiba ya Machi 24 asubuhi Mh. Majaliwa amesema mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli utaondoka Zanzibar asubuhi   na kuelekea Mkoani  Mwanza ambapo utatembea kwa gari kupitia daraja la Busisi na kusimama kwa dk 10 nyumbani kwa wazazi wa Mama Janeth Magufuli mjane wa Marehemu.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama amesema mapokezi ya leo Zanzibar yamedhihirisha umoja na mshikamano.

Amesema wa  Zanzibar wameudhihirishia ulimwengu kuwa Tanzania bara na Zanzibar ni ndugu wa damu ambapo amesema Mwenyezi Mungu awabariki wananchi wa pande zote mbili za muungano ili mshikamano uzidi baina ya Nchi hizo mbili.