Dodoma FM

Dodoma Jiji yaikabili Biashara

17 March 2021, 1:39 pm

Na Matereka Junior

Wakati ligi kuu bara ikiwa imesimama kupisha timu ya Taifa iliyopo Kenya kujiandaa na mechi za kufuzu mataifa Afrika, AFCON, Ligi ya timu za vijana wa chini ya miaka 20 za timu zote za ligi kuu inashika kasi.

Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar kwa mabao 2-1, leo timu ya vijana ya Dodoma Jiji inacheza tena mchezo wa pili dhidi ya Biashara United.

Mchezo huo unachezwa uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.