Dodoma FM

Wafanyakazi waeleza matarajio yao kuelekea siku ya wafanyakazi (Mei mosi)

29 April 2021, 1:36 pm

Na; Benard Filbert.

Kuelekea maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei mosi matarajio ya wafanyakazi wengi nchini ni kuongezewa mishahara na kupandishwa madaraja ili kuboresha utendaji kazi kwa maslahi yao   na nchi.

Hayo yamesemwa na Bw.Yusuph Mhindi ambaye ni mmoja wa wafanyakazi nchini wakati akizungumza na Taswira ya habari juu ya umuhimu wa siku hii na matarajio yao.

Bw.Ramadhan Mwendwa ni katibu wa idara ya elimu Chama cha wafanyakazi RAAHU makao makuu ameiambia taswira ya habari kuwa kupandishwa madaraja pamoja na kuongezewa mishahara ni moja ya matarajio ya wafanyakazi walio wengi nchini kuelekea katika siku ya wafanyakazi meimosi.

Aidha Bw.Mwendwa amewataka wafanyakazi kuendelea kujiunga katika vyama vya wafanyakazi kwani ni muhimu licha ya baadhi yao kutokuona umuhimu wa vyama hivyo.

Tarehe mosi ya mwezi Mei kila mwaka hufanyika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani lengo likiwa kutambua mchango wa wafanyakazi katika maslahi ya Taifa.