Dodoma FM

Mradi wa maji Nzuguni wafikia asilimia 96

27 November 2023, 5:28 pm

Picha ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule akikagua tanki la maji .Picha na Seleman Kodima.

Hatua hii ni moja ya njia ya kukabiliana na changamoto ya maji katika jiji la Dodoma ambapo Mradi wa Maji nzuguni unatarajia kuongeza hali ya uzalishaji wa maji kwa asilimia 11 na kuwanufaisha wakazi zaidi ya Wakazi 37,929 katika kata ya Nzuguni.

Na Seleman Kodima.

Imeelezwa kuwa Mradi wa visima vya Maji kata ya Nzuguni umefika asilimia 96  ambapo zoezi la majaribio la Mradi huo  limeanza  katika baadhi ya mitaa ya kata hiyo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mkoa wa Dodoma Mhandisi Aron Joseph wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ya kutembelea Mradi huo wenye zaidi ya Visima vitano ndani ya kata ya Nzuguni jijini Dodoma.

Sauti ya Mhandisi Aron Joseph .
Picha ni Mkuu wa mkoa akipata maelezo wakati akikagua visima hivyo . Picha na Seleman Kodima.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya Mradi huo ,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,Rosemary Senyamule amesema ni matamanio ya serikali kuona jiji la dodoma linakuwa na maji ya uhakika hivyo hatua ya majaribio hayo ni mafanikio mojawapo ya serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ,Rosemary Senyamule.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabiri Shekimweri amepongeza Hatua ya Duwasa kubuni miradi mingine ya maji kwa uchimbaji wa Visima vitano vya maji ikiwa ni sambamba na kisima cha mfano cha Mita 300 ikiwa lengo ni kuongeza hali ya upatikanaji wa maji jijini Dodoma.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Alhaji Jabiri Shekimweri.