Dodoma FM

Wanaume wahimizwa kuhudhuria kliniki na wake zao

5 September 2023, 1:57 pm

Muuguzi kutoka zahanati ya Mkonze akizungumzia umuhimu wa wanaume kwanda na wenza wao cliniki.Picha na Richald Ezekiel.

Miongoni mwa sababu zinazotajwa kusababisha mwitikio mdogo kwa wanaume kuwasindikiza wenza wao kliniki ni pamoja na kukabiliwa na majukumu ya kila siku jambo ambalo linaweza kutatulika iwapo kila mmoja atatambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki na mwenza wake.

Na Richard Ezekiel.

Wakati wataalamu wa afya wakisisitiza umuhimu wa mama kuhudhuria kliniki na mwenzake ili kupatiwa ushauri wa namna ya kulea ujauzito baadhi ya wanaume jijini dodoma wamezitaja baadhi ya saabu zinazochangia mwamko mdogo wa kuambatana na wenza wao kliniki.

hayo yanajiri kufuatia wataalamu wa afya kusisitiza juu ya suala la ushiriki wa wanaume kuongozana na wake zao kuhudhuria kliniki.

Sauti za baadhi ya wanaume.
Picha ni sehemu ya kutolea dawa kwa wagonjwa katika zahanati ya Mkonze.Picha na Richald Ezekiel.

Wataalamu wa afya wamekuwa wakisisitiza jamii juu ya suala hilo huyu hapa muuguzi wa afya kutoka kituo cha afya mkonze akizungumza katika mahojiano na Dodoma tv anaeleza juu ya umuhimu wa suala hilo.

Sauti ya Mtaalamu wa Afya.