Dodoma FM

Baadhi ya wakazi wa Ihumwa wakosa uelewa juu ya alama za mipaka

6 May 2022, 3:05 pm

Na; Victor Chigwada.

Baadhi ya Wananchi wa Ihumwa wametajwa kuwa na uelewa mdogo juu ya utunzaji wa Mali na miundombinu inayowekwa na Serikali kwa lengo la kuwanufaisha wananchi.

Kutokana na hayo wananchi wa Ihumwa wamesisitizana juu ya suala la kulinda bikoni zitakazo wekwa na Serikali katika hatua ya upimaji wa viwanja.

Wamesema kuwa Kuna baadhi wamekuwa wakijichukulia maamuzi ya kung’oa bikoni wanazo zikuta katika mipaka ya maeneo yao bila kujua athari zake.

.

Aidha mtendaji wa serikali ya mtaa wa Ihumwa A Bi.Siwazuri Karikule amewaomba wananchi kuacha tabia ya kujichukulia maamuzi wenyewe hususani tabia ya kuvunja bikoni zilizo wekwa katika mipaka ya viwanja.

Bi.Karikule ameongeza kuwa suala hilo lipo kisheria hivyo atakae kamatwa kwa kosa la kung’oa Bikoni atalazimika kulipa kiasi Cha shilingi laki Saba na elfu hamsini au kifungo Cha miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

.

Ili kuepukana na sintofahamu  ya kung’oa na kuvunja bikoni ambazo zipo na huwekwa kisheria kwa kutenganisha mipaka ya viwanja vya makazi,taasisi na hata barabara vyema wananchi kupewa elimu juu ya umuhimu wa alama hizo