Dodoma FM

Halmashauri yahamisha mnada wa Msalato

5 March 2021, 1:28 pm

Na, Shani Nicholous,

Dodoma.

Mnada wa Msalato Dodoma

Halmashauri ya jiji la Dodoma imepanga kuuhamishia mnada wa Msalato pembezoni mwa Soko la Jobu Ndugai lililopo Kata ya Nzuguni.

Mpango huo umepangwa kutekelezwa kabla ya nusu ya mwaka huu ambapo mnada huo unatarajiwa kuanzia juma lijalo kwa mujibu wa mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bw.Joseph Mafuru.

Amesema hatua hiyo haitaathiri mnada wa Msalato kwa kuuhamishia siku ya Jumapili.

Hata hivyo Bw.Mafuru amesema kuwa uwepo wa kituo kikuu cha mabasi ni miungoni mwa sababu zitakazovutia biashara kukua kwa kasi na watu kukutana kwa haraka zaidi.

Kwaupande wao wananchi jijini hapa wameipongeza Serikali kwa mipango hiyo kwani ni moja kati ya mbinu za kukuza biashara na hata kutengeneza fursa mpya za biashara na ajira kwa vijana.