Dodoma FM

KIBAWASA kutekeleza mradi wa maji Kibaigwa

14 April 2021, 12:04 pm

Na; Benard Filbert.

Imeelezwa kuwa  endapo mradi mpya wa maji ambao unatekelezwa katika mji mdogo wa Kibaigwa utakamilika utasiaidia kuondoa tatizo la maji kwa wakazi wa eneo hilo.

Hayo yameelezwa na afisa uhusiano kutoka mamlaka ya maji Kibaigwa Water Sanitation (KIBAWASA) Bw.Oscar Bakar wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu kukamilika kwa mradi mpya wa maji.

Amesema matarajio ya mamlaka hiyo baada ya kukamilika kwa mradi huo ni kuondoa changamoto zote ambazo wananchi wamekuwa wakilalamikia hususani kupata huduma ya maji kwa muda mfupi.

Kadhalika ameongeza kuwa wameomba fedha kutoka Wizara ya maji na Umwagiliaji na endapo zitapatikana kwa wakati hadi kufika mwezi Julai mwaka huu watakuwa wamekamilisha mradi huo.

Amewaomba wananchi kuwa wavumilivu kwani lengo lao ni kuwasaidia wakazi wa maeneo hayo kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.

Kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo ya mji wa Kibaigwa huku serikali ikiwekeza nguvu katika kutatua tatizo hilo ili kuwaletea unafuu wananchi.