Dodoma FM

Serikali kuanza ujenzi wa barabara ya Mpwampwa kwa kiwango cha lami

21 December 2023, 5:23 pm

Picha ni wajumbe wa kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika Jijini Dodoma.Picha na Yussuph Hassan.

Hii ni kufatia hoja ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Goerge Fuime kubiua hoja ya ujenzi wa barabara hiyo katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika leo Jijini Dodoma.

Na Arafa Waziri.
Hatimae kilio cha Wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma kimefikia tamati baada ya Serikali kuahidi kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami mwishoni mwa mwaka huu.
Mh George amesema kuwa barabara hiyo imekua kilio cha mda mrefu kwa wakazi wa mpwapwa.

Sauti ya mh. Goerge Fuime

Akijibia hoja hiyo Meneja Tanroads Mkoa wa Dodoma Leonard Chimagu amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo utaanza mwishoni mwa mwaka huu huku injinia Mkoa wa Dodoma akitaja maazimio yaliyofikiwa ndani ya kikao hicho.

Sauti ya Bw. Leonard Chimagu

Nae Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amesisitiza juu ya utekelezaji wa maazimio hayo.

Sauti ya Mh.Rosemary Senyamule .