Dodoma FM

Wakulima washauriwa kupanda mbegu zinazokomaa mapema

2 December 2020, 9:56 am

Moja ya mashamba ya mtama yaliyostawi vizuri

Na Benard Filbert,

Dodoma.

Kufuatia kunyesha kwa mvua za wastani mwaka huu wakulima Mkoani Dodoma wamehimizwa kutumia mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi hali itakayowasaidia kuepuka kupata mavuno hafifu.

Wito huo umetolewa na mkuu wa idara ya kilimo kutoka Mji wa Kondoa Bw.Hassan Kiseto wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu vitu vya kuzingatia kuelekea msimu wa kilimo kwa wakulima.

Amesema kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa kutoka mamlaka hali ya hewa nchini mvua za masika mwaka huu zitakuwa za wastani hivyo kila mkulima anatakiwa kuhakikisha anazingatia kupanda mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi.

Aidha, wakulima wamesisitizwa kufuatilia vyombo vya habari muda wote ili kupata taarifa mbalimbali ambazo zitawasaidia katika shughuli zao za kilimo.