Dodoma FM

Ifahamu dawa aina ya PEP

13 April 2023, 3:53 pm

Pep hupewa mtu ambaye anahisiwa kuambukizwa VVU hivi karibuni. Picha na Yussuph Hassan.

Hii ni njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa mtu asiye na VVU ambaye anaweza kuwa ameambukizwa virusi hivi

Na Yussuph Hassan.

Tunaendelea na mfululizo wa kuzungumzia juu ya dawa kinga za VVU, Prep na Pep, na leo Afisa Tabibu kutoka Zahanati ya Makole Glory Martine leo anazungumzia juu ya dawa kinga za VVU aina ya Pep, hii ni njia ya kuzuia maambukizi ya VVU kwa mtu asiye na VVU ambaye anaweza kuwa ameambukizwa virusi hivi karibuni ambapo atahitaji kupatiwa dawa ndani ya saa 72.

Matumizi ya dawa kinga dhidi ya VVU zipo mbili ambazo ni Prep na Pep, PrEP ni matumizi ya dawa za kupunguza makali ya VVU na watu wasio na VVU ili kuzuia upatikanaji wa maambukizi ya VVU na Pep hupewa mtu ambaye anahisiwa kuambukizwa VVU hivi karibuni.