Dodoma FM

Wananchi Majeleko walalamika kucheleweshewa fedha za fidia

15 February 2024, 4:01 pm

Wapo baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa na mradi huo wameshafanyiwa malipo .Picha na Portal.

Mradi BBT umebeba program ya ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo ambapo ilizinduliwa mnano Agosti 3-2022 na kuanza majaribio katika mikoa ya miwili ya Dodoma na Mbeya .

Na Victor Chigwada.
Wakazi wa kata ya Majeleko wilayani Chamwino wamelalamika kucheleweshewa fedha za fidia baada ya kupisha mradi wa BBT .

Hatua hii inajiri baada ya uthamini kukamilika na baadhi ya wananchi wakiwa tayari wamefanyiwa malipo yao huku ulipaji wa makundi mengine ukindelea kwa mwendo wa kusuasua.

Baadhi ya Wananchi wa kata hiyo wakizungumza na Taswira ya Habari wamesema wapo baadhi ya wananchi ambao maeneo yao yalichukuliwa na mradi huo wameshafanyiwa malipo .

Sauti za wananchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chinangali one Bw.Sephano Kamoga amesema kuwa kutokana na kucheleweshwa kwa malipo hayo wananchi wamekuwa wakiwalaumu viongozi wa serikali za mtaa.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Chinangali one Bw.Sephano Kamoga .

Nae Musa omary ambaye ni Diwani wa Kata hiyo amesema kuwa tayari suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi hivyo muda sio mrefu wananchi watakamilishiwa stahiki zao.

Sauti ya Musa omary ambaye ni Diwani wa Kata hiyo .

Aidha Taswira ya Habari inaendelea na jitahada za kuwatafuta Wasimamizi wa Mradi huo ambao ni wizara ya Kilimo kufahamu ni hatua zipi wanafanya kukamilisha malipo ya wananchi hao