Dodoma FM

Wawekezaji wazidi kuongezeka Dodoma

25 July 2023, 1:26 pm

Picha ni bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika duka la mwekezaji huyu linalojulikana kama Discount Center. Picha na Thadei Tesha.

Watu mbalimbali wanakaribishwa kuwekeza katika jiji la Dodoma kwani kuna fursa mbalimbali za uwekezaji.

Na Thadei Tesha.

Kufuatia kukua kwa jiji la Dodoma pamoja na ongezeko la watu kumepelekea wawekezaji mbalimbali kupata fursa ya kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu.

Bw. Salim Abdala ni mwekezaji kutoka jijini Dar-es-Salaam ambaye amekuja kuwekeza katika biashara ya mapambo na urembo wa nyumbani hapa anaeleza sababu iliyomsukuma kuja kuwekeza katika jiji la Dodoma.

Sauti ya Bw. Salim Abdala.
Bw Salim Abdala ni mwekezaji kutoka jijini Dar-es-Salaam ambaye amekuja kuwekeza katika biashara ya mapambo na urembo wa nyumbani.

Aidha anatoa wito kwa wafanyabiashara wengine kuja kuwekeza jijini Dodoma kutokana na uwepo wa fursa mbalimbali

Sauti ya Bw. Salim Abdala.

Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wamebainisha baadhi ya fursa za uwekezaji zilizopo katika jiji la Dodoma huku wakisema kuwa miongoni mwa sababu zinazopelekea kushindwa kuwekeza ni pamoja na ukosefu wa elimu pamoja na mitaji.

Sauti ya baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma.