Dodoma FM

DCEA yawaandaa wanafunzi kupambana na dawa za kulevya

10 October 2024, 7:01 pm

Na Mindi Joseph.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inawaandaa wanafunzi kupambana dhidi ya dawa za kulevya.

Akizungumza katika mdahalo uliowakutanisha wanafunzi na wadau wengine Oktoba 10 mwaka huu jijini Dodoma , Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kati,Mzee Kasuwi amewataka wanafunzi kuwa mabalozi wazuri kupambana dhidi ya dawa za kulevya.

Kamishna Msaidizi wa Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA),Kanda ya Kati ,Mzee Kasuwi
Sauti ya Mzee Kasuwi

Mwenyekiti wa sekretarieti ya mdahalo Wilaya ya Dodoma Mhandisi Francisco Magoha anasema mdahalo huo unawafunza watoto kutambua haki zao na wajibu kwani watoto wengi hawajui haki hizo.

Pichani Mwenyekiti wa sekretarieti ya Mdahalo Wilaya ya Dodoma Mhandisi Francisco Magoha
Sauti ya Mhandisi Francisco Magoha

Miongoni mwa wanafunzi walioshiriki mdahalo huo wameahidi kuwa mabalozi wazuri kwa jamii inayowazunguka.

Sauti za wananfunzi

Ushirikiano baina ya DCEA na TAKUKURU utajikita zaidi katika utoaji wa elimu juu ya tatizo la dawa za kulevya na kupiga vita rushwa kwa wanafunzi kuanzia shule za msingi Sekondarihadi vyuoni.