Dodoma FM

Kumaliza kifamilia matukio ya ukatili kunaathiri vipi upatikanaji wa haki

1 July 2026, 17:16

Wakati huu dunia inaposisitiza haki kwa wanawake, wasichana na watoto inakumbusha kupinga ukatili kwa kuzingatia Siku 16 za Kupinga Ukatili Kijinsia.Picha na mtandao.

Kwa hiyo mzizi ni sheria, kama ya ndoa ambayo inaruhusu binti wa chini ya miaka 14 kuozwa kwa kibali cha mahakama, mzazi au mlezi.

Unyanyasaji na ukatili kijinsia unaohusisha kutelekeza familia, vipigo, watoto kuozwa, kuingiliwa kinyume cha maumbile, mimba utotoni, kunyanyasa wanawake wenye VVU, kuua wazee kwa kusingizia wachawi ni tatizo mijini na vijijini.

Taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu ukatili wa kijinsia inaonyesha kuwa wanapokea malalamiko mengi kwenye madawati ya kijinsia na kwenye ripoti zinazofikishwa vituo mbalimbali.

Maelezo hayo yalionesha kuwa kuanzia Januari hadi Desemba 2023 matukio ya unyanyasaji kijinsia na ukatili yalikuwa 22,147 kwa watu wazima.

Wanawake walionyanyaswa walikuwa 13,322 wakati wanaume walikuwa 8,825 . Ripoti ya polisi inasema kuna ongezeko wakati mwaka 2022 kipindi kama hicho yalikuwa 18,403 ziada inaoneka 2023 kwa kuwa na matukio 3,744.

Ripoti inasema kuna ongezeko kubwa la unyanyasaji kijinsia kwa watoto mengi yakifanyika ndani ya familia na kwenye jamii pia. Yanahusisha kuuawa, unajisi- ulawiti, kubaka, mimba za utotoni na vipigo kupindukia.

Wakati huu dunia inaposisitiza haki kwa wanawake, wasichana na watoto inakumbusha kupinga ukatili kwa kuzingatia Siku 16 za Kupinga Ukatili Kijinsia, ukirejea kwanini ukatili unakithiri kuwepo mimba za utotoni licha ya jitihada za kutoa elimu kuhusu ulinzi wa watoto, kuwafundisha kujitetea na kujilinda sheria zinaendelea kuwa kikwazo.