Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuendelea kuchangia  damu

11 August 2026, 17:42

Picha ni District Governor wa Rotary International anayehudumu Tanzania na Uganda, Daniel Mukasa Ddamulira, alipofanya ziara katika Rotary Club ya Mwalimu Nyerere Dodoma.Picha na Bennard Filbert.

Ziara hiyo ililenga pia kuhamasisha jamii, hususani vijana, kutambua umuhimu wa kuchangia damu na kushiriki katika kuokoa maisha.

Na Bennard Filbert.

Jamii imetakiwa kuendelea kujitokeza na kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa damu katika maeneo mbalimbali nchini.

Wito huo umetolewa na District Governor wa Rotary International anayehudumu Tanzania na Uganda, Daniel Mukasa Ddamulira, alipofanya ziara katika Rotary Club ya Mwalimu Nyerere Dodoma.

Katika ziara hiyo, Daniel Mukasa alitembelea Hospitaliya Wilaya ya Bahi pamoja na Shule ya Sekondari Bihawana, ambapo lilifanyika zoezi la uchangiaji damu kwa wanafunzi kwa lengo la kuongeza akiba ya damu na kusaidia wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo.

Sauti ya Daniel Mukasa Ddamulira,
Picha ni wakati wa ziara katika Rotary Club ya Mwalimu Nyerere Dodoma.Picha na Bennard Komba.

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji Damu Kanda ya Kati, Dkt. Leah Kitundya, ameishukuru Rotary Club ya Mwalimu Nyerere Dodoma kwa mchango wake katika kuhamasisha jamii kujitokeza kuchangia damu, akieleza kuwa mahitaji ya damu bado ni makubwa katika jamii.

Sauti ya Dkt. Leah Kitundya.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule yaSekondari Bihawana wameishukuru Rotary kwa kuandaa zoezi hilo, wakieleza kuwa uchangiaji damu ni muhimu katika kusaidia kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.

Sauti za wanafunzi

Rotary Sunset Club imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya kijamii, ikiwemo uanzishaji na uhamasishaji wa klabu za damu nchini Tanzania na Uganda.