Wananchi watakiwa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao
8 June 2026, 17:53

Suma Jkt Marathon imeendelea kuwa moja ya matukio makubwa ya kijamii na kuhusisha washiriki mbali mbali kwa kulenga kuhamasisha afya bora na kuchangia ustawi wa jamii ambapo zaidi ya sh.million 100 zimepatikana katika mbio hizo na kuelekezwa kusaidia katika hospital.
Na Jerome John.
Wananchi Mkoani Dodoma wametakiwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha afya zao na kujikinga na magonjwa nyemelezi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Jacob Mkunda katika hitimisho la mbio za hisani zilizofahamika kama Suma Jkt Marathon 2026 zilizowakutanisha washiriki mbali mabali kutoka Dodoma.
Jenerali Mkunda amesema kuwa mazoezi ni sehemu ya tiba katika maisha ya mwanadamu kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama shinikizo la damu,kisukari na mengineyo ambayo yanaweza kumdhohofisha mtu na kumfanya kutofikia ndoto zake.

Aidha amebainisha kuwa mbali na mazoezi kumkinga mtu dhidi ya maradhi pia nia sehemu ya fursa ya kukutana,kufahamiana na kujenga mahusiano yanayochangia maendeleo ya jamii.
Kwaupande wa wananchi walioshiriki mbio hizo wamezishauri taasisi za umma naza binafsi nchini kuendelea kuandaa matamasha kama hayo ilikuwaleta watu pamoja na kuhusika katika kuchangia mahitaji ya kijamii kama kuchangia damu salama na kufanya usafi katika taasisi za umma kama hospital na nyinginezo.