Dodoma FM

Utawala bora kuchochea utatuzi bora wa migogoro

27 May 2026, 16:16

Picha ni mafunzo ya Uraia na Utawala Bora yanayotolewa kwa viongozi wa ngazi za mitaa, vijiji, kata, tarafa, halmashauri pamoja na kamati ya usalama ya wilaya.Picha na Mtandao.

Naye mmoja wa wakufunzi, Nickson Maleko, ameeleza baadhi ya maoni na mrejesho uliotolewa na washiriki wakati wa mafunzo hayo.

Na Mariam Kasawa.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Sophia Kizigo, amesema wilaya hiyo ni miongoni mwa maeneo yanayokabiliwa na migogoro ya ardhi, hali inayohitaji ujuzi na mbinu bora kwa viongozi ili kuweza kuitatua kwa ufanisi.

Amesema hayo baada ya kufungua mafunzo ya Uraia na Utawala Bora yanayotolewa kwa viongozi wa ngazi za mitaa, vijiji, kata, tarafa, halmashauri pamoja na kamati ya usalama ya wilaya, kupitia Wizara ya Katiba na Sheria.

Kizigo amesema mafunzo hayo yatawasaidia viongozi kuongeza ufanisi katika kushughulikia na kutatua migogoro inayojitokeza katika maeneo yao.

Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Mkuu na mratibu wa mafunzo hayo, Joyce Mushi, ameeleza tathmini ya utekelezaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika halmashauri zote nane za mkoa wa Dodoma.

Mshiriki wa mafunzo hayo, Rehema Mpangala ambaye ni mtendaji wa Kijiji cha Igunga, amekiri kuwepo kwa migogoro ya ardhi katika maeneo yao, akisema wanajitahidi kuishughulikia na kwamba mafunzo hayo yatawasaidia kuongeza ufanisi katika utatuzi wake.

Sauti ya Sophia Kizigo,