Wasio julikana waiba milango ya vyoo vya shule
19 June 2026, 18:12

Halmashauri ilitenga fedha na kukamilisha ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika Shule ya Msingi Ubembeni.
Na Kitana Hamis.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Mhe. Saidi Majaliwa, amesema Halmashauri ilitenga fedha na kukamilisha ujenzi wa vyoo vya wanafunzi katika Shule ya Msingi Ubembeni, ikiwa ni pamoja na kununua na kufunga milango ili kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Hata hivyo, amesema baada ya mradi huo kukamilika na kuanza kutumiwa na wanafunzi, baadhi ya watu wasio na nia njema walivamia na kuiba milango ya vyoo hivyo, kitendo kilichosababisha uharibifu wa miundombinu hiyo.
Majaliwa amelaani tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola kulinda mali za umma pamoja na kutoa taarifa za wahusika ili wachukuliwe hatua za kisheria.