Dodoma FM

Madereva watakiwa kuacha matumizi ya simu wanapokuwa barabarani

11 August 2026, 17:52

Matumizi ya simu wakati wa kuendesha chombo cha moto kimekuwa chanzo cha ajali barabarani. Picha na mtandao

Wananchi wameomba elimu ya usalama barabarani iendelee kutolewa kwa madereva na wamiliki wa vyombo binafsi vya usafiri, huku madereva wakihimizwa kuwasiliana kwa simu kabla ya kuanza safari ili kuhakikisha usalama wao na wa watumiaji wengine wa barabara.

Na Daniel Njau.

Wananchi na waendesha vyombo vya usafiri wametakiwa kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani, ikiwemo kuepuka matumizi ya simu wanapokuwa safarini, ili kupunguza ajali zinazoweza kusababishwa na uzembe wa madereva.

Baadhi ya wananchi wamesema matumizi ya simu wakati wa kuendesha yanaweza kumfanya dereva kupoteza umakini na kushindwa kufanya maamuzi ya haraka pindi anapokutana na hali inayoweza kusababisha ajali.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Askari wa Usalama Barabarani Bwana Lameck Julius, amesema Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168, inamtaka dereva kuepuka uzembe wakati wa kuendesha, huku hatua za kisheria zikijumuisha onyo na kufungiwa leseni ya udereva kwa muda wa miezi sita.

Sauti na Daniel Njau.