Dodoma FM

Mafunzo kwa vitendo yaandaa wanafunzi kwa soko la ajira

14 September 2026, 11:54

Mwanafunzi akiwa katika mafunzo ya vitendo. Picha na mtandao

Wanafunzi wametakiwa kutumia muda wa mafunzo kwa vitendo kujifunza kwa bidii, kuzingatia maadili ya kazi na kuuliza maswali wanapokutana na changamoto, ili kuongeza uelewa wao wa taaluma na kuwa tayari zaidi kwa soko la ajira.

Na Mathias Mgale.

Mafunzo kwa vitendo yameelezwa kuwa muhimu kwa wanafunzi wa vyuo katika kuwaandaa kukabiliana na mazingira halisi ya kazi baada ya kumaliza masomo, kwa kuwasaidia kupata uzoefu, kujenga kujiamini na kujifunza namna ya kutatua changamoto mbalimbali za kikazi.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Bi. Rehema Stephano, amesema mafunzo hayo huwasaidia wanafunzi kuunganisha nadharia wanazojifunza darasani na utekelezaji wake katika mazingira halisi ya kazi, hali inayowaongezea ujuzi, uzoefu na uwezo wa kufanya kazi.

Sauti ya Mathias mgale.