Wananchi wasisitizwa kuzingatia usafi kuepuka magonjwa, ihumnwa
31 August 2026, 17:51

Baadhi ya wananchi wamekiri uwepo wa maji tiririka ambayo kuhatarisha maisha ya watoto huku ikiwa ni wajibu wa Kila mtu kulinda usalama wa mazingira sambamba na Serikali kuweka miundombinu mizuri ya maji taka.
Na Victor Chigwada.
Wananchi wa mitaa ya Ihumwa wametakiwa kuzingatia usafi ili kuepukana na mlipuko wa magonjwa unaoweza kuhatarisha afya zao.
Hayo yameelezwa na mtaalamu wa afya Kata ya Ihumwa Bi.Shufaa Mohamed ambapo amesema kuwa wapo watu ambao wamekuwa hawana utamaduni wa kunawa mikono baada ya kutoka chooni ,na kuweka mazingira safi wakati wa kuandaa chakula sanjali na kula vyakula vilivyo lala pasipo kuvipasha .
Amewataka wananchi kuchukua tahadhali ya matumizi ya maji Kwa kuyachemsha kabla ya kutumia kwani Kinga ni bora kuliko tiba.