Miundombinu duni yaathiri upatikanaji wa elimu Mlodaa
18 September 2026, 16:23

Wazazi wameiomba Serikali kushughulikia changamoto ya uhaba wa walimu, upungufu wa madawati, ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na vyumba vya madarasa katika eneo hilo.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa ukosefu wa nyumba za walimu, uchakavu wa vyumba vya madarasa na upungufu wa madawati katika Kijiji cha Mlodaa, Wilaya ya Chamwino, vinaathiri ufanisi na ubora wa elimu na ufundishaji kwa wanafunzi.
Changamoto ya kukosekana kwa nyumba za walimu, madawati, uhaba wa walimu na majengo mazuri, hasa katika maeneo ya vijijini, huathiri moja kwa moja ufanisi na ubora wa ufundishaji kwa wanafunzi.
Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Mlodaa wilayani Chamwino, ambao wamesema kukosekana kwa nyumba za walimu kunapelekea walimu kuishi mbali na eneo la shule, hali inayosababisha walimu hao kukosa muda wa kuandaa masomo na kufanya kazi za ziada na wanafunzi wao.