Dodoma FM

Wazazi watakiwa kuthamini usawa kwenye elimu ya watoto wao

15 April 2026, 5:30 pm

Watoto wakike wengi hasa vijijini wanashindwa kupata haki ya kupata elimu kutokana na shule kuwa mbali.Picha na Haki Elimu.

Licha ya changamoto mbalimbali lakini kumekuwa na muamko mkubwa  ndani ya jamii wa kuwapeleka watoto wa kike shuleni pasipo kukatishwa masomo hususani maeneo ya vijijini.

Na Victor Chigwada.

Jamii imetakiwa kutambua umuhimu wa elimu Kwa watoto wa kike ili kukuza usawa wa kijia kwa watoto wa kiume na wakike.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wazazi walipokuwa wakiongea na Dodoma Tv ambapo wamesema watoto wakike wengi hasa vijijini wanashindwa kupata haki ya kupata elimu kutokana na shule kuwa mbali hivyo njiani hukutana na vishawisi na kujikuta wakikatisha masomo yao.

Aidha wametoa wito Kwa wazazi wenzao kupambana na kuhakikisha wanawajibika ipasavyo kwani baadhi  ya watoto wa kike wamekuwa wanazidiwa na vishawishi baada ya mzazi kushindwa kuwajibika ipasavyo katika mahitaji ya shule

Sauti za wazazi.

Nao baadhi ya wasichana wamesema kuwa ni vyema Serikali kuchukua hatua Kali Kwa wazazi watakao kwamisha elimu Kwa mtoto wa kike kwani wanawanyima haki yao ya msingi.

Sauti za wadada.

Richard Kisubi afisa maendeleo wa Kata ya Ngh’ambaku amekiri uwepo wa mwitikio mzuri kwa watoto wa kike kwenda shuleni kwani wamekuwa wakiweka mikakati ya ufuatiliaji kuhakikisha Kila mtoto anayetakiwa kwenda shule anakwenda bila kikwazo chochote.

Sauti ya Richard Kisubi