Dodoma FM

Bei ya kabichi shambani yawaliza wafanyabiashara

8 May 2023, 4:54 pm

Baadhi ya wauzaji wa kabichi katika soko kuu Majengo Jijini Dodoma.Picha na Thadei Tesha.

kwa sasa wastani wa bei ya kabichi ni kuanzia shilingi 1500 hadi 2000 huku wachache wakiuza kwa bei kati ya shilingi 1000 hadi 1500 kwa kabichi moja.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wafanyabiashara wa Mboga mboga aina ya kabichi Jijini Dodoma wamesema kwa sasa upatikanaji wa bidhaa hiyo sokoni bado si wa kuridhisha pamoja na kuwa kipindi hiki ni msimu wa upatikanaji wa bidhaa hiyo.

Dodoma Tv imewatembelea baadhi ya wafanyabiashara wa bidhaa hiyo  ambapo wanasema kuwa upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa sasa umekuwa mgumu kutokana na changamoto ya bei kutoka kwa wakulima mashambani.

Sauti za wafanyabiashara.
Mfanyabiashara wa kabichi Majengo Sokoni akizungumza na Dodoma Tv. Picha na Thadei Tesha.

Wafanyabiashara hao wameongeza kuwa kutokana na changamoto hiyo imepelekea bidhaa hiyo kutokuwa kwa wingi sokoni pamoja na kuuzwa kwa gharama kubwa tofauti na kipindi kingine msimu kama huu.

Sauti za Wafanyabiashara.