Dodoma FM

Ukosefu wa zahanati Mbelezungu Chamwino wapelekea vifo vya akina mama wajawazito

11 July 2023, 6:08 pm

kukosekana kwa zahanati katika kijiji hicho kunachangia baadhi ya akina mama wajawazito kupoteza maisha kutokana na umbali wa upatikanaji wa  huduma ya mama na mtoto. Picha na Victor Chigwada.

Sera ya afya ya mwaka 2007  imeweka wazi kuwa kila kijiji kanatakiwa kuwa na zahanati moja ili kuhudumia wananchi wa eneo hilo.

Na Victor Chigwada.

Imeelezwa kuwa ukosefu wa Zahanati katika kijiji cha Mbelezungu Wilayani Chamwino ni sababu inayosababisha vifo vya  akina mama wajawazito .

Hayo yamebainika baada ya kituo hiki kuzungumza na wakazi wa eneo hilo ambapo wamesema kukosekana kwa zahanati katika kijiji hicho kunachangia baadhi ya akina mama wajawazito kupoteza maisha kutokana na umbali wa upatikanaji wa  huduma ya mama na mtoto .

Sauti za wananchi.

Akizungumzia Changamoto hiyo  Diwani wa Kata hiyo   Bw.Musa Omary amekiri uwepo wa Zahanati mbili katika  Kata  hiyo hali ambayo bado ni changamoto kwa wananchi wanaokaa mbali na maeneo yanayopatikana zahanati hizo

Sauti ya Diwani

Kwa upande mwingine Diwani Huyo amesema kuwa licha ya uwepo wa zahanati hizo mbili lakini wanaupungufu wa wahuduma wa afya hali inayosababisha msongamano wagonjwa kwa nyakati tofauti

Sauti ya Diwani.